Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
Mwanzo 22:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Malaika wa BWANA akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, Biblia Habari Njema - BHND Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni, Neno: Bibilia Takatifu Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita Ibrahimu kutoka mbinguni mara ya pili, Neno: Maandiko Matakatifu Basi malaika wa bwana akamwita Ibrahimu kutoka mbinguni mara ya pili, BIBLIA KISWAHILI Malaika wa BWANA akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni |
Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.
akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.
Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.
Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Abrahamu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo.
Katika siku hiyo BWANA atawalinda wenyeji wa Yerusalemu; na yeye aliye dhaifu miongoni mwao atakuwa kama Daudi siku hiyo; nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama malaika wa BWANA mbele yao.
Hata miaka arubaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima wa Sinai katika muali wa moto, kichakani.
Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,
Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kulia kuelekea mbinguni,