Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.
Mwanzo 21:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Abrahamu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki nao wawili wakafanya agano baina yao. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki nao wawili wakafanya agano baina yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Abrahamu akachukua kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki nao wawili wakafanya agano baina yao. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo Ibrahimu akaleta kondoo na ng’ombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo Ibrahimu akaleta kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. BIBLIA KISWAHILI Abrahamu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano. |
Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.
Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu.
Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa.
Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
akawatwaa baadhi ya wazao wa kifalme; kisha akafanya agano naye, akamwapisha; akawaondoa watu wa nchi wenye nguvu;
Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.