Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Mwanzo 19:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

akawaambia, “Ndugu zangu, nawasihi msitende uovu huo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

akawaambia, “Ndugu zangu, nawasihi msitende uovu huo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

akawaambia, “Ndugu zangu, nawasihi msitende uovu huo.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Akawaambia, “La hasha, rafiki zangu! Msifanye jambo hili ovu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

akasema, “La hasha, rafiki zangu. Msifanye jambo hili ovu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Mwanzo 19:7
13 Marejeleo ya Msalaba  

Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.


Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.


Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mwanamume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.


Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.


Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.


Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;


Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.


Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.


Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.


Naye mwenye nyumba akawatokea hapo nje, na kuwaambia, La, sivyo, ndugu zangu nawasihi msifanye uovu jinsi hii; kwa kuwa mtu huyu ameingia ndani ya nyumba yangu, msifanye upumbavu huu.


Kisha Gaali, mwana wa Ebedi, akaenda pamoja na nduguze, wakavuka na kufika Shekemu; na watu wa Shekemu wakawa na imani naye.