Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Mwanzo 19:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao. Biblia Habari Njema - BHND Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hivyo, binti wote wawili wa Loti wakapata mimba kutokana na baba yao. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo binti wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Neno: Maandiko Matakatifu Hivyo binti wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. BIBLIA KISWAHILI Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. |
Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.
Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mwanamume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
BWANA akaniambia, Usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.
Adoni-bezeki akasema, Wafalme sabini, waliokuwa wamekatwa vidole vyao vya gumba vya mikono na vya miguu, waliokota chakula chao chini ya meza yangu; kama nilivyofanya mimi, Mungu amenilipa vivyo hivyo. Wakamleta Yerusalemu naye akafa kuko.
Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.