Mwanzo 17:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu alipomaliza kusema naye, akaondoka kwa Abrahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Mungu alipomaliza kuongea, akamwacha Abrahamu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Mungu alipomaliza kuongea, akamwacha Abrahamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Mungu alipomaliza kuongea, akamwacha Abrahamu. Neno: Bibilia Takatifu Alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, Mungu akaondoka kwa Ibrahimu. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati alipomaliza kuzungumza na Ibrahimu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Ibrahimu. BIBLIA KISWAHILI Mungu alipomaliza kusema naye, akaondoka kwa Abrahamu. |
Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.
BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni.
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Kwa maana, ikawa, mara huo muali wa moto ulipopaa juu mbinguni kutoka pale madhabahuni, huyo malaika wa BWANA akapaa katika mwali wa moto wa madhabahu; nao Manoa na mkewe wakaangalia; wakaanguka kifudifudi.
Ndipo malaika wa BWANA akanyosha ncha ya fimbo ile iliyokuwa mkononi mwake, akaigusa ile nyama na ile mikate; moto ukatoka mwambani, ukaiteketeza ile nyama na mikate; malaika wa BWANA akaondoka mbele ya macho yake.