Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.
Mwanzo 16:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abramu alikuwa na umri wa miaka 86 wakati Hagari alipomzaa Ishmaeli. Biblia Habari Njema - BHND Abramu alikuwa na umri wa miaka 86 wakati Hagari alipomzaa Ishmaeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abramu alikuwa na umri wa miaka 86 wakati Hagari alipomzaa Ishmaeli. Neno: Bibilia Takatifu Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita Hajiri alipomzalia Ishmaeli. Neno: Maandiko Matakatifu Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli. BIBLIA KISWAHILI Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli. |
Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.
Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.
Kwa hiyo, baada ya Abramu kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani, Sarai mkewe Abramu alimtwaa Hajiri Mmisri, mjakazi wake, akampa Abramu mumewe, kama mke.
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake.
Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.