Mika 7:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonesha mambo ya ajabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama wakati ulipotutoa nchini Misri, utuoneshe tena maajabu yako. Biblia Habari Njema - BHND Kama wakati ulipotutoa nchini Misri, utuoneshe tena maajabu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama wakati ulipotutoa nchini Misri, utuoneshe tena maajabu yako. Neno: Bibilia Takatifu “Kama siku zile mlipotoka Misri, nitawaonesha maajabu yangu.” Neno: Maandiko Matakatifu “Kama siku zile mlipotoka Misri, nitawaonyesha maajabu yangu.” BIBLIA KISWAHILI Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonesha mambo ya ajabu. |
Nami nitaunyosha mkono wangu, na kuipiga Misri kwa ajabu zangu zote, nitakazofanya kati yake, kisha baadaye atawapa ruhusa kwenda.
Akasema, Tazama, nafanya agano; mbele ya watu wangu wote nitatenda miujiza, ya namna isiyotendeka katika dunia yote, wala katika taifa lolote; na watu wote ambao unakaa kati yao wataona kazi ya BWANA, kwa maana ni neno la kutisha nikutendalo.
Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki, watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile waliyotoka katika nchi ya Misri.
Si wewe uliyemkatakata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.