Mika 5:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu kwa mataifa yasiyonitii. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hasira na ghadhabu yangu, nitalipiza kisasi mataifa yote yasiyonitii.” Biblia Habari Njema - BHND Kwa hasira na ghadhabu yangu, nitalipiza kisasi mataifa yote yasiyonitii.” Neno: Bibilia Takatifu Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu, kwa mataifa ambayo hayajanitii.” Neno: Maandiko Matakatifu Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu juu ya mataifa ambayo hayajanitii.” BIBLIA KISWAHILI Nami nitajilipiza kisasi katika hasira na ghadhabu kwa mataifa yasiyonitii. |
Kwa hiyo, asema Bwana, BWANA wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitalipiza kisasi kwa adui zangu;
mimi nitawaandikia kuuawa kwa upanga, na ninyi nyote mtainama ili kuchinjwa; kwa sababu nilipoita hamkuitika; niliponena, hamkusikia; bali mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambo nisiyoyafurahia.
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwanasimba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyagakanyaga na kuraruararua, wala hakuna wa kuokoa.
Basi sasa, sikieni asemavyo BWANA; Simama, ujitetee mbele ya milima, vilima navyo na visikie sauti yako.
katika muali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;