Nawe utasema, Bwana MUNGU asema hivi; Mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja; mji ufanyao vinyago juu ya nafsi yake, ili ujitie unajisi!
Mika 3:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wanaoijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Biblia Habari Njema - BHND Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Neno: Bibilia Takatifu mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu. Neno: Maandiko Matakatifu mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu. BIBLIA KISWAHILI Wanaoijenga Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu. |
Nawe utasema, Bwana MUNGU asema hivi; Mji umwagao damu ndani yake, ili wakati wake upate kuja; mji ufanyao vinyago juu ya nafsi yake, ili ujitie unajisi!
Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.
Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.
wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.