Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Mika 1:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kwa hiyo mtaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hivyo, mnapaswa kuagana na kuwaacha wakazi wa Morasheth-gathi. Nao mji wa Akzibu hautawasaidia wafalme wa Israeli,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hivyo, mnapaswa kuagana na kuwaacha wakazi wa Morasheth-gathi. Nao mji wa Akzibu hautawasaidia wafalme wa Israeli,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hivyo, mnapaswa kuagana na kuwaacha wakazi wa Morasheth-gathi. Nao mji wa Akzibu hautawasaidia wafalme wa Israeli,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi za kuagana. Mji wa Akzibu utaonesha wazi udanganyifu kwa wafalme wa Israeli.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi za kuagana. Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu kwa wafalme wa Israeli.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa hiyo mtaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Mika 1:14
10 Marejeleo ya Msalaba  

Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.

Ahazi akatwaa fedha na dhahabu iliyoonekana katika nyumba ya BWANA, na katika hazina za nyumba ya mfalme, akazipeleka kwa mfalme wa Ashuru kuwa zawadi.

Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.

Ufunuo juu ya wanyama wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba angurumaye, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.

Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?

Keila, Akizibu na Maresha; miji tisa, pamoja na vijiji vyake.