Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
Mhubiri 8:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aishikaye amri hatajua neno baya; Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayetii amri hatapata madhara, na mwenye hekima atajua kuna wakati na njia. Biblia Habari Njema - BHND Anayetii amri hatapata madhara, na mwenye hekima atajua kuna wakati na njia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayetii amri hatapata madhara, na mwenye hekima atajua kuna wakati na njia. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika, moyo wa hekima utajua wakati mwafaka na jinsi ya kutenda. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika, moyo wa hekima utajua wakati muafaka na jinsi ya kutenda. BIBLIA KISWAHILI Aishikaye amri hatajua neno baya; Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu. |
Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
Lakini hao wakunga walikuwa wacha Mungu, hawakufanya kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale watoto wa kiume.
Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.
Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kulia; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa.
Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;
Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.