Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu.
Mhubiri 8:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mimi nilipotia moyo wangu katika kuijua hekima, na kuuona utumishi uliofanyika juu ya nchi, (maana kuna asiyepata usingizi kwa macho yake mchana wala usiku); Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila nilipojaribu kujua hekima na kuona yanayotendeka hapa duniani, niligundua kwamba unaweza kukaa macho mchana na usiku, Biblia Habari Njema - BHND Kila nilipojaribu kujua hekima na kuona yanayotendeka hapa duniani, niligundua kwamba unaweza kukaa macho mchana na usiku, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila nilipojaribu kujua hekima na kuona yanayotendeka hapa duniani, niligundua kwamba unaweza kukaa macho mchana na usiku, Neno: Bibilia Takatifu Nilipotafakari akilini mwangu ili nijue hekima na kuangalia kazi ya mwanadamu duniani, jinsi macho yake hayapati usingizi mchana wala usiku, Neno: Maandiko Matakatifu Nilipotafakari akilini mwangu ili nijue hekima na kuangalia kazi ya mwanadamu duniani, jinsi ambavyo macho yake hayapati usingizi mchana wala usiku, BIBLIA KISWAHILI Mimi nilipotia moyo wangu katika kuijua hekima, na kuuona utumishi uliofanyika juu ya nchi, (maana kuna asiyepata usingizi kwa macho yake mchana wala usiku); |
Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu.
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.
Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.
Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kufukuza upepo.
Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo nayo ni ubatili.
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Usingizi wake kibarua ni mtamu, awe amekula kidogo, au awe amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu.
Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.