Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
Mhubiri 7:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana, kicheko cha mpumbavu ni kama mlio wa miiba motoni. Hayo nayo ni bure kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Maana, kicheko cha mpumbavu ni kama mlio wa miiba motoni. Hayo nayo ni bure kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana, kicheko cha mpumbavu ni kama mlio wa miiba motoni. Hayo nayo ni bure kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Hili nalo pia ni ubatili. Neno: Maandiko Matakatifu Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Hili nalo pia ni ubatili. BIBLIA KISWAHILI Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili. |
Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.
Nami nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa vilio; nami nitatia nguo za magunia katika viuno vyote, na upara katika kila kichwa; nami nitayafanya haya kuwa kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
Abrahamu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo yako mema katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unateseka.
Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia.