Mhubiri 7:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tafakarini vema kazi yake Mungu; ni nani awezaye kunyosha alichopinda Mungu? Biblia Habari Njema - BHND Tafakarini vema kazi yake Mungu; ni nani awezaye kunyosha alichopinda Mungu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tafakarini vema kazi yake Mungu; ni nani awezaye kunyosha alichopinda Mungu? Neno: Bibilia Takatifu Tafakari kile Mungu alichokitenda: Nani awezaye kunyoosha kile ambacho yeye amekipinda? Neno: Maandiko Matakatifu Tafakari kile Mungu alichokitenda: Nani awezaye kunyoosha kile ambacho yeye amekipinda? BIBLIA KISWAHILI Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye? |
Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena; Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
basi, niliiona kazi yote ya Mungu, ya kuwa haifahamiki na mwanadamu kazi inayofanyika chini ya jua; kwa sababu hata mwanadamu akijisumbua kadiri awezavyo kuichunguza, hataiona; naam, zaidi ya hayo, hata ingawa mwenye hekima hadai anajua, wao hawawezi kuifahamu.
Maana BWANA wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na mvinyo, zote ziko katika karamu zao; lakini hawaiangalii kazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake.
na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?
Basi, ikiwa hamwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kujisumbua kwa ajili ya yale mengine?
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.