Mhubiri 7:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usiseme, Kwa nini siku za kale zilikuwa ni bora kuliko siku hizi? Maana si kwa hekima unauliza hili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?” Huulizi hivyo kwa kutumia hekima. Biblia Habari Njema - BHND Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?” Huulizi hivyo kwa kutumia hekima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiulize, “Kwa nini nyakati za kale zilikuwa bora kuliko za sasa?” Huulizi hivyo kwa kutumia hekima. Neno: Bibilia Takatifu Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo. Neno: Maandiko Matakatifu Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo. BIBLIA KISWAHILI Usiseme, Kwa nini siku za kale zilikuwa ni bora kuliko siku hizi? Maana si kwa hekima unauliza hili. |
BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.
Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.