Mhubiri 5:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo, mfalme akijishughulisha na kilimo ni manufaa kwa wananchi wote. Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo, mfalme akijishughulisha na kilimo ni manufaa kwa wananchi wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo, mfalme akijishughulisha na kilimo ni manufaa kwa wananchi wote. Neno: Bibilia Takatifu Mafanikio ya nchi ni kwa ajili ya wote, hata mfalme mwenyewe hufaidi kutoka mashambani. Neno: Maandiko Matakatifu Mafanikio ya nchi ni kwa ajili ya wote, hata mfalme mwenyewe hufaidi kutoka mashambani. BIBLIA KISWAHILI Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba. |
Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.
Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.
Kuna mtu aliye peke yake, wala hana mwenzi wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba nyongeza. Hayo pia ni ubatili.
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.