Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
Mhubiri 5:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Siku zake zote hula gizani, mwenye fadhaa nyingi, mwenye ugonjwa na uchungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliishi maisha yake yote katika giza na huzuni; katika mahangaiko, magonjwa na hasira. Biblia Habari Njema - BHND Aliishi maisha yake yote katika giza na huzuni; katika mahangaiko, magonjwa na hasira. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliishi maisha yake yote katika giza na huzuni; katika mahangaiko, magonjwa na hasira. Neno: Bibilia Takatifu Siku zake zote hula gizani, pamoja na fadhaa kubwa, mateso na hasira. Neno: Maandiko Matakatifu Siku zake zote hula gizani, pamoja na fadhaa kubwa, mateso na hasira. BIBLIA KISWAHILI Siku zake zote hula gizani, mwenye fadhaa nyingi, mwenye ugonjwa na uchungu. |
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
Naye akasema, Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie mwenyewe na mwanangu, tule kisha tufe.
Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.
Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Nendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, BWANA asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.
Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Kweli, watu wote hupita kama kivuli; Wao hujisumbua bure tu; Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.
Wala sikuyanyima macho yangu chochote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yoyote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.
Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo nayo ni ubatili.
Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo niliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.
Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.