Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Mhubiri 4:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, ambaye hasikilizi shauri jema;

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, ambaye hasikilizi shauri jema;

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, ambaye hasikilizi shauri jema;

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Mhubiri 4:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya.

Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Yupo mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza BWANA kwa yeye, yaani Mikaya mwana wa Imla; lakini namchukia; kwa sababu hanibashirii mema, ila mabaya. Yehoshafati akasema, La! Mfalme asiseme hivi.

Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.

Afadhali maskini aendaye katika uadilifu wake, Kuliko mpotovu wa midomo aliye mpumbavu.

Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotovu wa njia angawa ni tajiri.

Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watamstahimili; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Hekima ni nguvu zake mwenye hekima, Zaidi ya wakuu kumi waliomo mjini.