Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Mhubiri 12:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi Mhubiri nasema: Yote ni bure kabisa! Yote ni bure. Biblia Habari Njema - BHND Mimi Mhubiri nasema: Yote ni bure kabisa! Yote ni bure. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi Mhubiri nasema: Yote ni bure kabisa! Yote ni bure. Neno: Bibilia Takatifu Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili! Kila kitu ni ubatili!” Neno: Maandiko Matakatifu Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili! Kila kitu ni ubatili!” BIBLIA KISWAHILI Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili! |
Hakika binadamu ni ubatili, Na wenye cheo ni uongo, Katika mizani huinuka; Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.
Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kufukuza upepo.
Basi, nikauchukia uhai; kwa sababu kazi inayotendeka chini ya jua ilikuwa mbaya kwangu; yaani, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.
Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
Kwa maana ni nani ajuaye yaliyo mema ya mwanadamu katika maisha yake, siku zote za maisha yake ya ubatili, anayoishi kama kivuli? Kwa maana ni nani awezaye kumweleza mwanadamu mambo yatakayofuata baada yake chini ya jua?
Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuponyoka katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.