Akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.
Mhubiri 12:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati huo utaogopa kupanda mahali pa juu na kutembea barabarani ni kitisho; wakati miti ya mlozi inachanua na panzi wanashiba, lakini wewe hutakuwa na hamu tena. Wakati huo binadamu anapaswa kwenda katika makao yake ya milele, nao waombolezaji watapitapita barabarani. Biblia Habari Njema - BHND Wakati huo utaogopa kupanda mahali pa juu na kutembea barabarani ni kitisho; wakati miti ya mlozi inachanua na panzi wanashiba, lakini wewe hutakuwa na hamu tena. Wakati huo binadamu anapaswa kwenda katika makao yake ya milele, nao waombolezaji watapitapita barabarani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati huo utaogopa kupanda mahali pa juu na kutembea barabarani ni kitisho; wakati miti ya mlozi inachanua na panzi wanashiba, lakini wewe hutakuwa na hamu tena. Wakati huo binadamu anapaswa kwenda katika makao yake ya milele, nao waombolezaji watapitapita barabarani. Neno: Bibilia Takatifu wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu na hatari zitakazokuwepo barabarani; wakati mlozi utakapochanua maua na panzi kujikokota nawe usiwe na shauku ya kitu chochote. Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele nao waombolezaji wakizunguka barabarani. Neno: Maandiko Matakatifu wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu na hatari zitakazokuwepo barabarani; wakati mlozi utakapochanua maua na panzi kujikokota nawe usiwe na shauku ya kitu chochote. Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele nao waombolezaji wakizunguka barabarani. BIBLIA KISWAHILI Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani. |
Akasema, Mwanangu hatashuka pamoja nanyi, maana nduguye amekufa, naye amesalia peke yake; mabaya yakimpata katika njia mtakayoiendea ndipo mtakaposhusha mvi zangu kwa sikitiko mpaka kaburini.
Na mkiniondolea huyu naye, na madhara yakimpata, mtashusha mvi zangu kwa msiba kaburini.
itakuwa atakapoona ya kwamba huyu kijana hayuko, atakufa; na watumwa wako watashusha mvi za mtumwa wako, baba yetu, kwa huzuni kaburini.
Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, Niifikie nyumba waliyoaandaliwa wenye uhai wote.
Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.
Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi.
Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa.
Mwondokeeni mtu mwenye mvi; heshimuni uso wa mtu mzee; nawe mche Mungu wako, Mimi ndimi BWANA.