Mhubiri 11:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayengoja upepo hatapanda mbegu, anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu. Biblia Habari Njema - BHND Anayengoja upepo hatapanda mbegu, anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayengoja upepo hatapanda mbegu, anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote atazamaye upepo hatapanda, yeyote anayeangalia mawingu hatavuna. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote atazamaye upepo hatapanda, yeyote aangaliaye mawingu hatavuna. BIBLIA KISWAHILI Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna. |
Mawingu yakiwa yamejaa mvua, Yataimimina juu ya nchi; Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, Paangukapo ule mti, papo hapo utalala.
Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.