Mhubiri 10:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala: Biblia Habari Njema - BHND Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala: Neno: Bibilia Takatifu Kuna ubaya niliouona chini ya jua, aina ya kosa litokalo kwa mtawala: Neno: Maandiko Matakatifu Kuna ubaya niliouona chini ya jua, aina ya kosa litokalo kwa mtawala: BIBLIA KISWAHILI Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; |
Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu.
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Kuna balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima;
Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.