Basi kama vile baba yangu alivyowatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.
Mhubiri 10:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ole wako, nchi, iwapo mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ole wako, ewe nchi, mtawala wako akiwa kijana, na viongozi wako wakifanya sherehe asubuhi. Biblia Habari Njema - BHND Ole wako, ewe nchi, mtawala wako akiwa kijana, na viongozi wako wakifanya sherehe asubuhi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ole wako, ewe nchi, mtawala wako akiwa kijana, na viongozi wako wakifanya sherehe asubuhi. Neno: Bibilia Takatifu Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi. Neno: Maandiko Matakatifu Ole wako, ee nchi ambayo mfalme wako alikuwa mtumwa na ambayo wakuu wako hufanya karamu asubuhi. BIBLIA KISWAHILI Ole wako, nchi, iwapo mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi! |
Basi kama vile baba yangu alivyowatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.
Wakamkusanyikia watu mabaradhuli, wasiofaa kitu, waliojitia nguvu juu ya Rehoboamu mwana wa Sulemani, Rehoboamu alipokuwa kijana na wa moyo mwororo, asiweze kuwazuia.
Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja, alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja;
Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala; akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu.
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake.
Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA.
Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.
Kuhusu watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.
Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.