Tena akuoneshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.
Mhubiri 1:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kilichopindika hakiwezi kunyoshwa, kisichokuwapo hakiwezi kuhesabiwa. Biblia Habari Njema - BHND Kilichopindika hakiwezi kunyoshwa, kisichokuwapo hakiwezi kuhesabiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kilichopindika hakiwezi kunyoshwa, kisichokuwapo hakiwezi kuhesabiwa. Neno: Bibilia Takatifu Kilichopindika hakiwezi kunyooshwa; kile ambacho hakipo haiwezekani kukihesabu. Neno: Maandiko Matakatifu Kilichopindika hakiwezi kunyooshwa, kile ambacho hakipo haiwezekani kukihesabu. BIBLIA KISWAHILI Yaliyopotoka hayawezi kunyooshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki. |
Tena akuoneshe hizo siri za hekima, Ya kuwa hufanikiwa katika kuyatimiza makusudi yake! Ujue basi ya kuwa Mungu akuachilia katika uovu wako.
Akitoa utulivu yeye, ni nani awezaye kuhukumia makosa? Akificha uso wake, ni nani awezaye kumtazama? Kama hufanyiwa taifa, au mtu mmoja, ni sawasawa;
Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.
Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu.
Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipoinuka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa;
Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoadoa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.
na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?