Adui wameangamia na kuwa magofu milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea.
Mhubiri 1:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hakuna kumbukumbu lolote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lolote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakuna mtu anayekumbuka ya zamani wala atakayekumbuka yatakayotukia baadaye. Biblia Habari Njema - BHND Hakuna mtu anayekumbuka ya zamani wala atakayekumbuka yatakayotukia baadaye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakuna mtu anayekumbuka ya zamani wala atakayekumbuka yatakayotukia baadaye. Neno: Bibilia Takatifu Hakuna kumbukumbu ya watu wa zamani, hata na wale ambao hawajaja bado hawatakumbukwa na wale watakaofuata baadaye. Neno: Maandiko Matakatifu Hakuna kumbukumbu ya watu wa zamani, hata na wale ambao hawajaja bado hawatakumbukwa na wale watakaofuata baadaye. BIBLIA KISWAHILI Hakuna kumbukumbu lolote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lolote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye. |
Adui wameangamia na kuwa magofu milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea.
Je! Kuna jambo lolote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.
Maana hakuna kumbukumbu la milele la mwenye hekima, wala la mpumbavu; kwa sababu siku zijazo wote pia watakuwa wamekwisha kusahauliwa. Na mwenye hekima, jinsi gani anavyokufa sawasawa na mpumbavu!
Pia nikaona waovu wamezikwa, nao wamefika kaburini; tena waliofanya mema wameondoka katika patakatifu, nao wamesahauliwa mjini. Hayo nayo ni ubatili.
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana tuzo tena; maana hata kumbukumbu lao limesahauliwa.
Tazama, mambo ya kwanza yamekuwa, nami nayahubiri mambo mapya; kabla hayajatokea nawapasheni habari zake.