Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Ikiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?
Methali 8:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe, Na wao wanichukiao hupenda mauti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Asiyenipata anajidhuru mwenyewe; wote wanaonichukia wanapenda kifo.” Biblia Habari Njema - BHND Asiyenipata anajidhuru mwenyewe; wote wanaonichukia wanapenda kifo.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Asiyenipata anajidhuru mwenyewe; wote wanaonichukia wanapenda kifo.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini yeyote ashindwaye kunipata hujiumiza mwenyewe; na wote wanaonichukia mimi hupenda mauti.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini yeyote ashindwaye kunipata hujiumiza mwenyewe; na wote wanichukiao mimi hupenda mauti.” BIBLIA KISWAHILI Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe, Na wao wanichukiao hupenda mauti. |
Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake? Ikiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?
Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.
Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.
Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama BWANA alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli?
Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli?
Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona ninyi wenyewe kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.
Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tuko hapa.
Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
sisi je! Tutapataje kupona, tukipuuza wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliomsikia;