Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Methali 6:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake, wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake. Biblia Habari Njema - BHND Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake, wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usimtamani mwanamke huyo kwa uzuri wake, wala usikubali kunaswa kwa kope za macho yake. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wako usitamani uzuri wake, wala macho yake yasikuteke, Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke, BIBLIA KISWAHILI Usiutamani uzuri wake moyoni mwako; Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake. |
Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Umenishangaza moyo, dada yangu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, Kwa mtupo mmoja wa macho yako, Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.
Tena mmewatuma watu kuwaita watokao mbali; ambao mjumbe alitumwa kwao, na tazama, wakaja; nawe ulijiosha kwa ajili yao, ulitia rangi macho yako, na kuremba kwa mapambo mazuri;
lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.