Methali 4:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili. Biblia Habari Njema - BHND Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili. Neno: Bibilia Takatifu Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika. Neno: Maandiko Matakatifu Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika. BIBLIA KISWAHILI Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike; |
Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.
Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA, Na mienendo yake yote huitafakari.
Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.
mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.