Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Methali 31:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpe kileo mtu anayekufa, wape divai wale wenye huzuni tele; Biblia Habari Njema - BHND Mpe kileo mtu anayekufa, wape divai wale wenye huzuni tele; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpe kileo mtu anayekufa, wape divai wale wenye huzuni tele; Neno: Bibilia Takatifu Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu, Neno: Maandiko Matakatifu Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu, BIBLIA KISWAHILI Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. |
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia; Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.
Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.
Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.