Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Methali 31:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu. Biblia Habari Njema - BHND Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakinywa watasahau maagizo ya sheria, na kuwanyima haki wenye taabu. Neno: Bibilia Takatifu wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote waliodhulumiwa. Neno: Maandiko Matakatifu wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa. BIBLIA KISWAHILI Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. |
Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.
Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki; naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki; Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu.
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.