Nao farasi aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi, kila kundi na thamani yake.
Methali 31:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza, huwauzia wafanyabiashara mishipi. Biblia Habari Njema - BHND Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza, huwauzia wafanyabiashara mishipi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanamke huyo hutengeneza nguo na kuziuza, huwauzia wafanyabiashara mishipi. Neno: Bibilia Takatifu Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi. Neno: Maandiko Matakatifu Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza, naye huwauzia wafanyabiashara mishipi. BIBLIA KISWAHILI Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. |
Nao farasi aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi, kila kundi na thamani yake.
Shamu alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa kazi za mkono wako walifanya biashara kwa zumaridi, urujuani, kazi ya taraza, kitani safi, marijani na akiki, wapate vitu vyako vilivyouzwa.
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
Samsoni akawaambia, Mimi nitawategea ninyi kitendawili; kama mnaweza kunitegulia katika hizo siku saba za karamu, na kukitambua, ndipo nitakapowapa mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu;