Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
Methali 31:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mume wake ni mtu mashuhuri barazani, anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi. Biblia Habari Njema - BHND Mume wake ni mtu mashuhuri barazani, anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mume wake ni mtu mashuhuri barazani, anakoshiriki vikao vya wazee wa nchi. Neno: Bibilia Takatifu Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji, aketipo miongoni mwa wazee wa nchi. BIBLIA KISWAHILI Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. |
Wakati nilipotoka kwenda mjini, kupitia langoni, Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
Weka waamuzi na maofisa katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki.
ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake;
Basi Boazi akakwea kwenda mpaka langoni, akaketi pale; na tazama, yule mtu wa jamaa aliyekuwa karibu, ambaye Boazi amemnena, akapita. Naye akamwita, Haya! Wewe, karibu, uketi hapa. Naye akaja akaketi.
Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.
Kisha akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, Ninyi nanyi, ketini hapa. Wakaketi.