Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili.
Methali 31:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe, maana kila mmoja anazo nguo za kutosha. Biblia Habari Njema - BHND Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe, maana kila mmoja anazo nguo za kutosha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hawahofii watu wake ijapo baridi ya kipupwe, maana kila mmoja anazo nguo za kutosha. Neno: Bibilia Takatifu Theluji inaposhuka, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto. Neno: Maandiko Matakatifu Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto. BIBLIA KISWAHILI Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. |
Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili.
Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu.
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito, Ni kama yeye avuaye nguo wakati wa baridi; Ni kama siki juu ya magadi.
Magari ya vita yanafanya vishindo njiani, Yanasonganasongana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.