Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Methali 31:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua, na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake. Biblia Habari Njema - BHND Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua, na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hufikiria kununua shamba, kisha hulinunua, na kulima zabibu kwa faida ya jasho lake. Neno: Bibilia Takatifu Huangalia shamba na kulinunua; kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu. Neno: Maandiko Matakatifu Huangalia shamba na kulinunua, kutokana na mapato yake hupanda shamba la mizabibu. BIBLIA KISWAHILI Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. |
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Tena huamka, kabla usiku haujaisha; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, liko mbele yangu. Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako, Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.
Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.
Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini?