Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
Methali 31:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hutafuta sufu na kitani, na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii. Biblia Habari Njema - BHND Hutafuta sufu na kitani, na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hutafuta sufu na kitani, na kufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii. Neno: Bibilia Takatifu Huchagua sufu na kitani, naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii. Neno: Maandiko Matakatifu Huchagua sufu na kitani naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii. BIBLIA KISWAHILI Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake kwa moyo wote. |
Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
na awe ameshuhudiwa kwa matendo mema; katika kulea watoto, kuwa mkaribishaji, kuwaosha watakatifu miguu, kuwasaidia wateswao, na kujitolea kutenda wema katika hali zote.
Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, watunze nyumba zao; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.
na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
Hivyo yeye akafuatana na wasichana wake Boazi na kuokota, hadi mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano pia; naye alikuwa akikaa kwa mkwewe.