Methali 31:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mke mwema kweli, apatikana wapi? Huyo ana thamani kuliko johari! Biblia Habari Njema - BHND Mke mwema kweli, apatikana wapi? Huyo ana thamani kuliko johari! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mke mwema kweli, apatikana wapi? Huyo ana thamani kuliko johari! Neno: Bibilia Takatifu Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani. Neno: Maandiko Matakatifu Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani. BIBLIA KISWAHILI Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana thamani yake yapita thamani ya marijani. |
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
ambayo bado nafsi yangu ningali nikiitafuta, nisiione; mwanamume mmoja katika elfu nimemwona; bali mwanamke mmoja miongoni mwa wote mimi sikumwona.
Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa mkosa adabu na mwovu; naye alikuwa wa ukoo wa Kalebu.