Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Methali 30:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hatishwi na mwingine yeyote yule; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema simba: Mnyama mwenye nguvu kuliko wote, wala hamwogopi mnyama mwingine yeyote; Biblia Habari Njema - BHND simba: Mnyama mwenye nguvu kuliko wote, wala hamwogopi mnyama mwingine yeyote; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza simba: mnyama mwenye nguvu kuliko wote, wala hamwogopi mnyama mwingine yeyote; Neno: Bibilia Takatifu simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, wala haogopi chochote; Neno: Maandiko Matakatifu simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, asiyerudi nyuma kwa chochote; BIBLIA KISWAHILI Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hatishwi na mwingine yeyote yule; |
Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba.
Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.
Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya mataifa, kati ya kabila nyingi, mfano wa simba kati ya wanyama wa msituni, kama mwanasimba kati ya makundi ya kondoo, ambaye, akiwa anapita katikati, hukanyagakanyaga na kuraruararua, wala hakuna wa kuokoa.
Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.
Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu.