Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.
Methali 30:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kuna na wengine – kiburi ajabu! Hudharau kila kitu wanachokiona. Biblia Habari Njema - BHND Kuna na wengine – kiburi ajabu! Hudharau kila kitu wanachokiona. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kuna na wengine — kiburi ajabu! hudharau kila kitu wanachokiona. Neno: Bibilia Takatifu ambao daima macho yao ni ya kiburi, na kutazama kwao ni kwa dharau; Neno: Maandiko Matakatifu wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, ambao kutazama kwao ni kwa dharau; BIBLIA KISWAHILI Kuna kizazi cha watu ambao macho yao yameinuka kama nini! Na kope zao zimeinuka sana. |
Amsingiziaye jirani yake kwa siri, Huyo nitamwangamiza. Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno, Huyo sitamvumilia.
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala mambo yanayozidi nguvu zangu.
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa,
Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha.
Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.