Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.
Methali 3:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Biblia Habari Njema - BHND Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Neno: Bibilia Takatifu Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. Neno: Maandiko Matakatifu Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. BIBLIA KISWAHILI Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. |
Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.
Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka asubuhi huyafanya, sababu wana uwezo mikononi mwao.
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliokosa kuwalipa kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.