Methali 3:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu. Biblia Habari Njema - BHND Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukiketi hutakuwa na hofu; ukilala utapata usingizi mtamu. Neno: Bibilia Takatifu unapolala, hutaogopa; unapolala, usingizi wako utakuwa mtamu. Neno: Maandiko Matakatifu ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu. BIBLIA KISWAHILI Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu. |
Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama.
Usingizi wake kibarua ni mtamu, awe amekula kidogo, au awe amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.
Nami nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni.
Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapovunja vifungo vya nira zao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha.
Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala na hakuna atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.
Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakalilinda gereza.