Methali 29:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenye kumbembeleza jirani yake, anatega mtego wa kujinasa mwenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Mwenye kumbembeleza jirani yake, anatega mtego wa kujinasa mwenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenye kumbembeleza jirani yake, anatega mtego wa kujinasa mwenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. Neno: Maandiko Matakatifu Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. BIBLIA KISWAHILI Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. |
Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
Maana vinywani mwao hamna uaminifu; Moyo wao ni shimo tupu, koo lao ni kaburi wazi, Ulimi wao hujipendekeza.
Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
Toka juu amepeleka moto mifupani mwangu, Nao umeishinda; Ametandika wavu aninase miguu, Amenirudisha nyuma; Amenifanya kuwa mtu wa pekee, Na mgonjwa mchana kutwa.
Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.
Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.
Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote, kama mjuavyo, wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
Nao watumishi wa Sauli wakanena maneno hayo masikioni mwa Daudi. Daudi akasema, Je! Ninyi mnaona kuwa ni shani mimi kuwa mkwewe mfalme, nami ni maskini, tena sina cheo?