Methali 29:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu. Biblia Habari Njema - BHND Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mdhalimu ni chukizo kwa mnyofu, naye mnyofu ni chukizo kwa mwovu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki. BIBLIA KISWAHILI Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu. |
Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Maneno ya Aguri mwana wa Yake; mausia mtu huyu aliyomwambia Ithieli, naam, Ithieli na Ukali.
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.
Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.