Methali 29:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima. Biblia Habari Njema - BHND Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kiburi cha mtu humporomosha mwenyewe, lakini mnyenyekevu wa roho atapata heshima. Neno: Bibilia Takatifu Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima. Neno: Maandiko Matakatifu Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima. BIBLIA KISWAHILI Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. |
Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi.
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.
aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.