Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Methali 29:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika. Biblia Habari Njema - BHND Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika. Neno: Bibilia Takatifu Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. Neno: Maandiko Matakatifu Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. BIBLIA KISWAHILI Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua. |
Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.
Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawati na nyeupe, mwenye taji kubwa la dhahabu, na joho la kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Susa wakapaza sauti, wakashangilia.
Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa; Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji.
Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale majusi, alighadhibika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wa kiume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake kote, kuanzia wenye miaka miwili na chini yake, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale majusi.
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.