Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
Methali 28:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliye mkarimu kwa maskini hatatindikiwa kitu, lakini anayekataa kuwaangalia atalaaniwa kwa wingi. Biblia Habari Njema - BHND Aliye mkarimu kwa maskini hatatindikiwa kitu, lakini anayekataa kuwaangalia atalaaniwa kwa wingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliye mkarimu kwa maskini hatatindikiwa kitu, lakini anayekataa kuwaangalia atalaaniwa kwa wingi. Neno: Bibilia Takatifu Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi. BIBLIA KISWAHILI Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi. |
Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako.
Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;
Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.