Hazaeli akasema, Lakini mimi mtumwa wako ni nani, mimi niliye mbwa tu, hata nifanye jambo hili kubwa? Elisha akajibu, BWANA amenionesha ya kwamba wewe utakuwa mfalme juu ya Shamu.
Methali 28:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayetegemea akili yake mwenyewe ni mpumbavu; lakini anayeishi kwa hekima atakuwa salama. Biblia Habari Njema - BHND Anayetegemea akili yake mwenyewe ni mpumbavu; lakini anayeishi kwa hekima atakuwa salama. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayetegemea akili yake mwenyewe ni mpumbavu; lakini anayeishi kwa hekima atakuwa salama. Neno: Bibilia Takatifu Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye ajitumainiaye mwenyewe ni mpumbavu, bali yeye atembeaye katika hekima hulindwa salama. BIBLIA KISWAHILI Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa. |
Hazaeli akasema, Lakini mimi mtumwa wako ni nani, mimi niliye mbwa tu, hata nifanye jambo hili kubwa? Elisha akajibu, BWANA amenionesha ya kwamba wewe utakuwa mfalme juu ya Shamu.
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.