Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Methali 28:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye BWANA ataneemeshwa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mchoyo huchochea ugomvi, lakini anayemtegemea Mwenyezi-Mungu atafanikiwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mchoyo huchochea ugomvi, lakini anayemtegemea Mwenyezi-Mungu atafanikiwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mchoyo huchochea ugomvi, lakini anayemtegemea Mwenyezi-Mungu atafanikiwa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye Mwenyezi Mungu atafanikiwa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mtu mwenye tamaa huchochea fitina, bali yule amtegemeaye bwana atafanikiwa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina; Bali amtumainiye BWANA ataneemeshwa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Methali 28:25
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.


Kuchukiana huleta fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote.


BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.


Nafsi ya mtu mkarimu itastawishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.


Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana.


Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; Bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.


Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.


Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.


Mng'ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa.


Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.


Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma.


Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.


Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.


Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.


Lakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.