Mifupa yangu yote itasema, BWANA, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini kutoka kwa mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Methali 28:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Anayeiba mali ya baba yake au mama yake, akasema si kosa, hana tofauti yoyote na wezi wengine. Biblia Habari Njema - BHND Anayeiba mali ya baba yake au mama yake, akasema si kosa, hana tofauti yoyote na wezi wengine. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Anayeiba mali ya baba yake au mama yake, akasema si kosa, hana tofauti yoyote na wezi wengine. Neno: Bibilia Takatifu Yeye amwibiaye babaye au mamaye na kusema, “Si kosa,” yeye ni mwenzi wa yule aharibuye. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye amwibiaye babaye au mamaye na kusema, “Si kosa,” yeye ni mwenzi wa yule aharibuye. BIBLIA KISWAHILI Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu. |
Mifupa yangu yote itasema, BWANA, ni nani aliye kama Wewe? Umponyaye maskini kutoka kwa mtu aliye hodari kumshinda yeye, Naam, maskini na mhitaji na mtu amtekaye.
Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima; Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.
Naye akamwambia mama yake, Hizo fedha elfu na mia moja ulizoibiwa, na kuweka laana kwa ajili yake na kusema masikioni mwangu, tazama, ninazo mimi hizo fedha; ni mimi niliyezitwaa. Mama yake akasema, Mwanangu na abarikiwe na BWANA.