ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Methali 28:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwaminifu atapata baraka tele, lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwaminifu atapata baraka tele, lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwaminifu atapata baraka tele, lakini mwenye pupa ya kuwa tajiri hataepa adhabu. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka hataacha kuadhibiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mwaminifu atabarikiwa sana, bali yeye atamaniye kupata utajiri kwa haraka hataacha kuadhibiwa. BIBLIA KISWAHILI Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa. |
ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi, Hao wakae nami. Yeye aendaye katika njia kamilifu, Ndiye atakayenitumikia.
Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi.
Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?
Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
Tena, aliwaambia wanafunzi wake, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake.
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.
Ninapajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe unalishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Basi Ahimeleki akamjibu mfalme, akasema, Katika watumishi wako wote ni nani aliye mwaminifu kama Daudi, aliye mkwewe mfalme, tena msiri wako, mwenye heshima nyumbani mwako?