Methali 28:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu, atakuwa mkimbizi mpaka kaburini; mtu yeyote na asijaribu kumzuia. Biblia Habari Njema - BHND Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu, atakuwa mkimbizi mpaka kaburini; mtu yeyote na asijaribu kumzuia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu, atakuwa mkimbizi mpaka kaburini; mtu yeyote na asijaribu kumzuia. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro hadi kufa; mtu yeyote asimsaidie. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mwenye kusumbuliwa na hatia ya kuua atakuwa mtoro mpaka kufa; mtu yeyote na asimsaidie. BIBLIA KISWAHILI Aliyelemewa na damu ya mtu Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie. |
Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.
Lakini Absalomu akakimbia. Na kijana yule aliyekuwa mlinzi akainua macho yake, akaona, na tazama, kuna watu wengi wanakuja kwa njia ya upande wa kilima nyuma yake.
Kisha vijana kumi, waliomchukulia Yoabu silaha zake wakamzunguka, wakampiga Absalomu, na kumwua.
Akaambiwa mfalme Sulemani ya kwamba, Yoabu amekimbilia Hemani kwa BWANA, naye, tazama, yuko madhabahuni. Ndipo Sulemani akamtuma Benaya, mwana wa Yehoyada, akisema, Nenda, umuue.
Ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, BWANA asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.
Tena BWANA alinena habari za Yezebeli, akisema, Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli.
Hakika, jana nimeiona damu ya Nabothi, na damu ya wanawe, asema BWANA; nami nitakulipa katika kiwanja hiki, asema BWANA. Basi sasa mtwae huyu ukamtupe katika kiwanja hicho, sawasawa na neno la BWANA.
Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe.
Lakini Ishmaeli, mwana wa Nethania, akatoroka pamoja na watu wanane, Yohana asimpate, akawaendea wana wa Amoni.
Wenyeji walipomwona yule nyoka akilewalewa mkononi, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni mwuaji; ambaye ijapokuwa ameokoka katika bahari haki haimwachi kuishi.
Lakini mtu awaye yote akimchukia mwenziwe na kumwotea na kumwinukia, akampiga hata akafa; naye akakimbilia miji hii mmojawapo;